| Author |
Message |
mwanabongo
Member

Joined: 20 Dec 2004
Posts: 20

|
Posted:
Tue Jan 04, 2005 5:49 am Post subject: KIONGOZI GANI KWA TANZANIA 2005? |
  |
Asalam Aleikhum mabibi na mabwana na ninawatakia kheri na fanaka za mwaka mpya wa 2005. Baada ya kuwaza na kuwazua tunapoufungulia mwaka huu nimeona nitoe mawazo yangu juu ya jambo moja la muhimu linalotukabili mwaka huu. Uchaguzi mkuu wa Rais na Wabunge utafanyika Oktoba mwaka huu. Watanzania watapata nafasi kuondoa madarakani, kurejesha au kuwaingiza vipya viongozi wao kwa nji ya kura na si mtutu au mapinduzi! Ni matumaini yangu kuwa uchaguzi utafanyika mara moja bila kasoro nyingi. Na ni mategemeo yangu kuwa uchaguzi huo utakuwa huru na wa haki.
Ninachotolea mawazo leo siyo uchaguzi wenyewe bali ni yule Kiongozi wa Taifa ambaye ataliongoza Taifa letu kwa miaka ijayo mitano.
Kiongozi huyo ni wa namna gani na kwanini?
Katika miongo iliyopita tulijaliwa kuwa na viongozi ambao wameiwezesha nchi yetu kubakia moja (Territorial Integrity) na kuendelea kuwa na amani (Tranquility). Hayo yalifikiwa chini ya uongozi wa MJKN na chini ya utawala wa AHM na chini ya Rais anayemaliza muda wake BWM.
Tanzania ya 2005 haihitaji kiongozi kama hao, tunahitaji kiongozi mwenye sifa za hao wote na si chini ya hapo. Hizo sifa ni zipi na kwanini tunazihitaji?
Kiongozi tunayehitaji kati ya sifa nyingi kubwa ni hii:Awe ni mwenye maono (Visionary) na awe mwenye kuhamasisha umma (Charismatic).
a. Mwenye maono (Visionary)
Tanzania haitaji kiongozi anayekubalika na chama fulani cha siasa au mwenye elimu ya aina aina au mtu ambaye ni mtendaji tu. Taifa letu linahitaji mtu mwenye kuona mbali na anayejua ni wapi anataka kulipeleka Taifa letu. Historia inaonyesha kuwa kila Taifa lililofanikiwa katika muda fulani wa historia inatokana na uwepo wa kiongozi mwenye maono aliyeweza kuona mbali na wapi anataka Taifa lake lifike. MJKN alikuwa ni mtu wa namna hiyo, mnakumbuka yale maneno ya "sisi tunataka kuwasha Mwenge..."? au wakati kutangaza vita dhidi ya Idi Amin " Sababu ya kumpiga tunayo..."? Mwalimu alikuwa na maono. Maono ninayozungumza hapa siyo yale ya kidini bali ni yale yanatokana na uelewa wa kiongozi huyo kuhusu ndoto na matamanio ya watu wake.
Watanzania wanatamani mambo kadhaa, Elimu nzuri na yenye ushindani, Afya bora na mfumo mzuri wa Afya ya Raia, Usalama wa mali na nafsi zao. Maisha mazuri na ya kisasa. Kila nyumba kuwa na umeme, maji safi, kumudu usafiri unaotegemewa n.k Haya ni matamanio ya watu wetu. Ni kiongozi gani anayeweza kutuongoza kufikia hayo? Je Lipumba, Kikwete, Malecela, nk wana maono yoyote au wanataka kutekeleza ile "ilani ya uchaguzi"?
Hivyo basi, kiongozi yoyote anayekuja ni yule anayeweza kusema kama Martin Luther King Jr. "I have a Dream..."
b. Kiongozi Mhamasishaji
Kiongozi tunayetamka na haswa tunayemhitaji ni yule mwenye uwezo wa kuhamasisha na kushawishi watu. Siyo mwenye maneno ya ulaghai au utamu tu wa maneno. Ni kiongozi ambaye maneno yake yanawafanya watu waamini na wajiamini kuwa wanaweza kufanya mambo zaidi ya wanavyodhania. Waingereza walikuwa na Winston Churchill na Wamerekani wakati wa vita vya wenyewe walikuwa na Ab Lincoln na wakati wa mwanzo wa vita baridi walikuwa na JFK. Tulipopata uhuru tulikuwa na MJKN na Afrika Kusini walikuwa na Nelson Mandela. Je sisi tunaye mtu gani mwenye uwezo wa kushawishi kama hao? Je Lipumba, Mrema, Kikwete, Salim nk wanauwezo gani wa kushawishi? Na hapa sizungumzii ushawishi unaotokana na vitisho "ohh tusiposhinda damu itamwagika, ohh, msipokubali kushindwa mtaona nguvu ya dola, ohh, hili ama lile".
La hasha, ushawishi ninaozungumzia unatokana na nguvu za hoja na siyo hoja za Nguvu. Ni ushawishi utakaowafanya Watanzania, wainuke kutoka katika kuzoea umaskini na maisha duni na kuinuka kuelekea mafanikio, utajiri na maendeleo. Ni ushawishi utakoalifanya Taifa letu kuhesabiwa kuwa miongoni mwa Mataifa yalioendelea. Ni kiongozi anayeweza kusema kuwa "na sisi tunaweza". Kama Korea Kusini wameweza, India wameweza, Wachina wameweza, Brazil wameweza, iweje sisi tusiweze? Hivi sisi hatuna kitu gani ambacho wengine wanacho?
Hayo basi ndugu zangu hayo ndiyo mawazo niliyo nayo katika kufungulia mwaka huu.
Wabilahi Tawfiq! |
|
|
   |
 |
Times
Newbie

Joined: 01 Jan 2005
Posts: 11

|
Posted:
Tue Jan 04, 2005 8:59 am Post subject: |
  |
Ndugu,
Naona ungepanua zaidi Hoja yako kwani tupo Wa Tanzania Millioni 35 .hii ni ile ajenda kuwa Kuna Wanaouzoefo wa Kuongoza na SIISI TUNA UZOEFU WA KUONGOZWA.
Unaonaje RAIS akawa Pengo,Makamo Shaabani Simba na Waziri Mkuu Ask. Ramadhani? Unaonaje Rais akawa Balali ,Mkamo Leonard Tenga,Waziri Mkuu Reginal Mengi? Unaonaje Rais akawa Sarakikiya,Makamo Mahita,Waziri Mkuu Makamba?Sio lazima Rais atokee Kwenye Chama anaweza Rais kutoka Nje ya Chama kwani sasa tunayo INDEPENDENT CANDIDATE. |
|
|
   |
 |
mwanabongo
Member

Joined: 20 Dec 2004
Posts: 20

|
Posted:
Tue Jan 04, 2005 2:04 pm Post subject: |
  |
Times, Ingawa mahakama imekubali kimsingi hoja ya kuwa na mgombea binafsi, Bunge la Tanzania halijapitasha sheria hiyo. Hivyo basi, kama mtu anataka kugombea ni lazima atoke katika chama fulani cha siasa. Hao uliowataja je ni visionaries? Je wanauwezo wa kushawishi wananchi, kwa kutumia hoja za kisiasa na siyo za kidini? |
|
|
   |
 |
Times
Newbie

Joined: 01 Jan 2005
Posts: 11

|
Posted:
Tue Jan 04, 2005 4:26 pm Post subject: |
  |
Kutumia Hoja za Siasa sio kazi kubwa.Hapa kwetu hakuna Siasa kwa maana ya Siasa bali kuna wale ambao tumewatanguliza or choosen people. |
|
|
   |
 |
mtoto wa mjini
Member

Joined: 30 Dec 2004
Posts: 21

Age: 50
|
Posted:
Tue Jan 04, 2005 6:53 pm Post subject: |
  |
yaani kutokana na vielelezo ulivyovitaja hapo juu...bado mimi sijaona kiongozi hapo bongo mwenye hizo sifa...labda tukamtafute south africa mana ndio tunakokimbiliaga wakati tunatafuta watu wa kuongoza vitega uchumi vyetu |
|
|
      |
 |
mwanabongo
Member

Joined: 20 Dec 2004
Posts: 20

|
Posted:
Wed Jan 05, 2005 3:18 am Post subject: |
  |
Miye nadhani yupo, tatizo ni kuwa hawa CCM na Wapinzani wanatutia kiwingu na tunashindwa kumtambua. |
|
|
   |
 |
Times
Newbie

Joined: 01 Jan 2005
Posts: 11

|
Posted:
Wed Jan 05, 2005 7:11 am Post subject: |
  |
.Leo tuna Deni la 10billion Dollars.Wakati huo WA UHURU Dollar ilikuwa shs 7 leo Dollar shs 1000.Kazi ya kutawala Nchi inataka KUWA TUMEKUWA NA technology NA SCIENCE .HUWEZI UKACHONGA UKASEMA HUYU RAIS.AFADHALI TUFUTE UCHAGUZI MPAKA TUUTAKAPOWEZA KUWA NA UCHUMI IMARA NDIPO TUUFANYE.WAKATI WA MWALIMU TULISOMA BURE LEO TUNALIPA FEDHA KIBAO IFM ,BUSINESS COLLEGE N.K |
|
|
   |
 |
Domitila
Regular Member

Joined: 22 Dec 2004
Posts: 83
Location: BONGO

Age: 35
|
Posted:
Wed Jan 05, 2005 9:12 am Post subject: |
  |
Times wrote: .Leo tuna Deni la 10billion Dollars.Wakati huo WA UHURU Dollar ilikuwa shs 7 leo Dollar shs 1000.Kazi ya kutawala Nchi inataka KUWA TUMEKUWA NA technology NA SCIENCE .HUWEZI UKACHONGA UKASEMA HUYU RAIS.AFADHALI TUFUTE UCHAGUZI MPAKA TUUTAKAPOWEZA KUWA NA UCHUMI IMARA NDIPO TUUFANYE.WAKATI WA MWALIMU TULISOMA BURE LEO TUNALIPA FEDHA KIBAO IFM ,BUSINESS COLLEGE N.K
Kwa maana hiyo Times unachokisema ni kuwa tukiachie Chama Tawala kitengeneze uchumi wetu hadi hapo utakapokuwa Imara ndipo tufanye uchaguzi. Sasa kuna uwezekano kweli wa viongozi wa sasa kutuletea huo uchumi imara?? Kwa sababu kama nimemwelewa vema wa mjini anasema hakuna kiongozi afaaye kuwa rais ..... sasa hawa watakaoweza kutuletea uchumi imara wapo kweli??  |
|
|
   |
 |
mwanabongo
Member

Joined: 20 Dec 2004
Posts: 20

|
Posted:
Wed Jan 05, 2005 4:01 pm Post subject: |
  |
Miye ninachosema ni kuwa huu mtindo wa vyama vya siasa unatunyima viongozi wenye maono na wahamasishaji. Kwani majina ya wote wanaotajwa ni watu ambao wako tayari kutekeleza sera na itikadi za vyama vyao. Lakini, nichopendekeza kwa mwaka huu ni kiongozi awezaye kwenda juu na zaidi ya sera na itikadi (above and beyond ideology and policies)!! Sijui ni nani, mrema ni mhamasishaji lakini hana maono, Lipumba ana maono (tatizo ya maono yake yana umwagaji damu), ccm wana maono hawana wahamasishaji (kama wapi hawapewi nafasi ya kujitokeza). This is what the Americans call Catch 22 |
|
|
   |
 |
Domitila
Regular Member

Joined: 22 Dec 2004
Posts: 83
Location: BONGO

Age: 35
|
Posted:
Wed Jan 05, 2005 5:33 pm Post subject: |
  |
Mwanabongo umesema kuwa vyama vya siasa vyatunyima viongozi wenye maono kwa sababu wao wanafata itikadi na sera za vyama vyao... pengine mie sielewi vizuri (hasa ukizingatia kuwa siasa is not one of my favourate ) kwani haiwezekani hayo maono yakawa moja ya sera na itikadi ya vyama?? kwani nilidhani kuwa chama ni nyenzo tu ya kupitishia mtazamo wako juu ya uongozi au hali fulani ya siasa.  |
|
|
   |
 |
|
|
|
|